BAADA ya kutoka nchini Msumbiji akiwa hoi, msanii wa vichekesho
Bongo, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ hatimaye amepata nguvu na ameanza
kujikongoja katika kazi ya uigizaji.
Akichonga
na paparazi wetu hivi karibuni, Matumaini alisema kwa sasa anaendelea
vizuri na ameshaanza kucheza filamu mbalimbali anazoshirikishwa na
wasanii wenzake na sasa anaendesha maisha yake mwenyewe.
“Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani kama siyo wao, ningerudishwa nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atakayewalipa,” alisema Matumaini.
“Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani kama siyo wao, ningerudishwa nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atakayewalipa,” alisema Matumaini.
Matumaini alivyokuwa alipotoka Msumbiji.
Hata hivyo, alilaani vikali baadhi ya wasanii wanaozusha maneno ya
uongo kwamba Michael Sangu alikula fedha alizokuwa anachangisha kwa
ajili yake jambo ambalo siyo la kweli.