Wema (katikati) akiomba dua na wenzake wakati wa futari aliyoiandaa nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar.
Imelda Mtema na Hamida Hassan
NI yuleyule Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa mara nyingine anatengeneza kichwa cha habari baada ya kufanya kufuru ‘funga kazi’ kwenye futari aliyoiandaa nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar na kuwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa, Amani ndani ya nyumba.
AALIKA WATOTO YATIMA
Katika futari hiyo iliyofanyika Jumatatu wiki hii, Wema aliwaalika watoto yatima ambao ndiyo lilikuwa chaguo lake la kwanza kisha watu wa kawaida ambao hawana majina na mastaa mbalimbali Bongo.NA GLOBAL PUBLISHER
WEMA AKARIBISHA WAGENI
Muda mwingi Wema alionekana akipita huku na kule kukaribisha wageni waliokuwa wakiingia katika lango kuu la nyumbani kwake na kuhakikisha kila mtu anapata sehemu ya kukaa.
VYAKULA VYA KUMWAGA
Futari aliyoiandaa staa huyo ilikuwa na vyakula vingi vilivyopelekwa na magari kabla ya kushushwa na kupangwa sehemu mbili tofauti, sehemu ya wanawake na wanaume.
WATU WALA, WASAZA
Katika mnuso huo, watu walinawa maji ya chupa tofauti na futari za mastaa wengine ambao hunawisha wageni maji ya bombani.
Wingi wa vyakula uliwafanya waalikwa wale, wanywe hadi kusaza kwani kila sahani ilipakiwa chakula kibao huku kingine kikibaki.
MASTAA WABEBA
Baada ya kula vyakula na vingine kubaki kwenye sahani zao, baadhi ya mastaa walioalikwa, walienda kununua mifuko ya plastiki na ‘foili’ kisha wakaweka vyakula walivyobakisha na kuondoka navyo.
Staa ambaye hakujificha wakati anaweka chakula hicho kwenye mifuko ni Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ambaye alisema kuliko kumwaga bora abebe akale daku.
Staa mwingine ambaye hakujificha, ni Mtangazaji wa Runinga ya Channel Ten, Salma Msangi ambaye kifurushi chake alikiweka mbele kabisa.
Kama ilivyokuwa wakati wa kuanza kula, baada ya kumaliza watu walinawa maji ya chupa na kuifanya futari hiyo kuonekana funga kazi.
KAWAZIBA MIDOMO AKINA DIAMOND?
Wakati Amani linafungasha virago eneo la tukio, kuliibuka madai kuwa inawezekana Wema alifanya hivyo ili kuwaziba midomo mastaa ambao wameshafuturisha kama Nasibu Abdul ‘Diamond’, Salma Jabu ‘Nisha’ na Mboni Masimba.