KESI ya kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao Meneja wa
Hoteli, Goodluck Kuyumbu inayomkabili Staa wa Filamu, Wema Isaac Sepetu
imeunguruma Jumatano iliyopita katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar
na watu kufurika pomoni, Ijumaa linakumegea kilichojiri.
Katika mahakama hiyo watu walifurika kwa lengo la kutaka kumuona Wema
aliyepandishwa mbele ya Hakimu, Bernice Ikanda kusomewa mashtaka ya
kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana
Goodluck.
ATINGA NA MSAFARA
Wakati wa kuwasili mahakanai hapo, Wema aliambatana na msafara wa magari
matatu, yeye akiwa katika lake la aina ya Audi Q 7, magari mengine
yalikuwa ni Toyota Opa na Toyota Hiace yaliyokuwa na watu wake.
WATU WAFURIKA MAHAKAMANI
Kutokana na jamii kupenda kufuatilia matukio ya kila siku ya Wema, watu kibao walifika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo.
Mara baada ya mlimbwende huyo wa mwaka 2006-07 kuzama katika chumba cha
mahakama, kulitokea vurugu kwa baadhi ya watu kukanyagana ili kutaka
kumuona na kusikilza kesi hiyo kwa ukaribu zaidi.
AINGIZWA CHUMBA CHA MAHAKAMA
Wema aliingizwa katika chumba cha mahakama sambamba na Goodluck ambapo
Hakimu Bernice alianza kumuuliza mlalamikaji kama alikuwa na mashahidi
walioshuhudia tukio hilo lilivyotokea.
Goodluck alijibu kuwa anao mashahidi na kumwambia hakimu kwamba anaweza kuwaleta mbele ya mahakama hiyo.
KESI YAPIGWA KALENDA TENA
Hakimu aliamuru kesi hiyo iahirishwe hadi Agosti 20, mwaka huu na kumtaka mlalamikaji kufika na mashahidi wake.
Kuonesha kwamba watu wengi walikuwa wamefika kushuhudia kesi hiyo, walitawanyika baada ya uamuzi huo.
WEMA ANUNUA MIHOGO
Mara baada ya kutoka mahakamani na kuruhusiwa kuondoka kutokana na
dhamana aliyonayo, Wema alionekana akinunua mihogo kwa ajili ya futari
ya siku hiyo.
Credit:GPL