Tuesday, July 2, 2013

PICHA ZA AJALI YA SAIBABA ILIYOTOKEA HAPO JANA













































watu 21 wamejeruhiwa vibaya na wengine 30 wakinusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Songea kupata ajali eneo la vigwaza mkoani pwani.

mkuu wa kikosi cha askari wa barabarani Chalinze Assistance Inspector Sule amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili asubuhi July 02 baada ya basi la abiria la kampuni ya Saibaba lenye namba za usajili T 779BKL kutaka kulipita gari lingine huku likiwa katika mwendo kasi na hatimaye gari lilimshinda dereva huyo na kisha kupinduka

Aidha ameongeza kuwa majeruhi hao wamekimbizwa katika hosiptali ya tumbi kibaha kwaajili ya matibabu,basi hilo lilikuwa na jumla ya abiria 51.