Wednesday, July 3, 2013

"WASANII WA BONGO MOVIE NI WEZI WA WAUME ZA WATU" AMANDA

MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amesema anawachukia sana wasanii wa kike wa Bongo Movie kutokana na tabia zao za kuchukuliana mabwana.
Amanda alisema wasanii wengi wa filamu wana tabia za kuibiana mabwana kitendo ambacho kinamkera na kusababisha kuwachukia kwani wanavyofanya siyo heshima na inawaharibia sifa kwa jamii pamoja na kuichafua tasnia yao kwa jumla.
“Nawachukia na ndiyo maana sitaki kuwa na rafiki Bongo Movie kwa sababu wamekuwa na tabia mbaya sana mifano halisi ipo lakini siwezi kuitaja,” alisema.

Mbali na hivyo, Amanda alisema kuna wasanii wawili wa kike walikuwa marafiki sana hata kwenye mitandao walikuwa wakiitana mawifi lakini hivi sasa hawaivi, kisa kunyang’anyana bwana