Thursday, July 11, 2013

ARSENAL YAMGEUKIA TENA KIUNGO WAKE WA ZAMANI CESC FABREGAS

KWA mara nyingine Arsenal inataka kumrejesha Nahodha wake wa zamani,Cesc Fabregas majira ha ya joto. 

Kwa sasa kiungo huyo wa zamani wa The Gunners yupo mapumzikoni baada ya kumaliza kuichezea Hispania kwenye Kombe la Mabara na mustakabali wake Barcelona haueleweki kutokana na msimu mbaya uliopita. 

Taarifa nchini Hispania zimeendelea kusema atabaki Nou Camp, lakini shaka inaletwa na namna atakavyoingia kwenye mipango ya kocha Tito Vilanova baada ya msimu uliopita kutemwa katika mechi zote kubwa.


Cesc Fabregas



Dili la kumsajili tena Fabregas halitakuwa na utata, kwa sababu wakati Arsenal inamuuza mchezaji huyo Hispania kwa Pauni Milioni 25, ilipewa nafasi ya kwanza ya kumsajili ikimhitaji. 

Ikiwa Barca itaamua kumuuza Fabregas, The Gunners watapewa nafasi ya kwanza ya kumsajili kwa Pauni Milioni 25.

Wakati huo huo: The Gunners imefufua mpango wa kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams kufuatia Thomas Vermaelen kurejea kwenye maumivu. 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales ni mtu anayetakiwa mno na Arsene Wenger majira haya joto, lakini Arsenal haijafika bei ya dau la Pauni Milioni 10 linalotakiwa kwa ajili ya beki huyo. 

Nahodha Vermaelen anaweza akakosa maandalizi ya mwanzoni mwa msimu kutokana na kuumia tena, na ataiacha Gunners na mabeki wawili tu walio fiti; Laurent Koscielny na Per Mertesacker.

Thomas Vermaelen
Ashley Williams