club mbili ambazo ni mahasimu wakubwa ktk jiji la Manchester MAN U na Man City wameingia katika vita kubwa kuwania saini ya mshambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic mwenye thamani ya pauni milioni 27.
Bosi mpya wa United David Moyes amegeukia kwa nyota huyo wa kimataifa wa Montenegro baada ya kushindwa kumshawishi mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski.
Ni habari mbaya kwa bosi wa City, Manuel Pellegrini, ambaye alikuwa akiamini tayari wamemtia mkobani mshambuliaji huyo.
Wakala wa Jovetic, Fali Ramadani alikuwa London wiki hii baada ya Fiorentina kutoa ruksa ya mazungumzo na wanunuzi.
Fiorentina wiki hii ilimsaini Mario Gomez kwa pauni milioni 15 kutoka Bayern Munich.
Jovetic, 23, kwenye mkataba wake ana kifungu kinachomruhusu kuondoka kwa ada ya pauni milioni 27.
City waliweka wazi kuwa wao wako tayari kufikia kiwango hicho cha ada kwa mshambuliaji huyo ambaye alifunga mabao 13 katika Serie A msimu uliopita na ambaye pia alicheza katika mchezo wa sare ya 1-1 dhidi Uingereza mwezi Machi.
Lakini United sasa wako tayari kufikia ofa ya mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki huku ikiamini mfumo wao utamvutia zaidi Jovetic.