WATOTO sita, wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru walikopelekwa kwa matibabu na kuangaliwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, watoto hao walidai kufanyiwa mchezo huo kwa nyakati tofauti na wachungaji watatu wa kanisa hilo lililopo eneo la Feed Force, Kwamorombo jijini Arusha.
Mmoja wa watoto hao anayesoma darasa la 4 katika shule ya msingi alieleza kuwa yeye na wenzake wamekuwa wakifanyiwa mchezo mchafu katika kanisa hilo baada ya wachungaji hao kuwapatia shilingi 2,000 za kufungia mdomo.
“Siku moja nilipofika shuleni wenzangu wakaniambia niende pale kanisani tukapewe hela, nilipofika niliwaona wenzangu wengine wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname akanifanyia kitendo kibaya na kunipa shilingi 2,000, niliumia sana,’’ alisema mwanafunzi mmoja.
Mwanafunzi mwingine alisema amekuwa akitoroka shuleni na wenzake na kwenda kwa watumishi hao ambapo huwaingiza katika kanisa hilo na kujifanya wanawaombea baadaye huwafanyia mchezo mbaya.
Mwanafunzi mwingine alisema amekuwa akitoroka shuleni na wenzake na kwenda kwa watumishi hao ambapo huwaingiza katika kanisa hilo na kujifanya wanawaombea baadaye huwafanyia mchezo mbaya.
“Tukifika huwa wanatufungia ndani na kutuambia tuwanyonye, baadaye wanatubaka na wakimaliza wanatuambia tukisema kwa mtu yeyote watatuchinja na kutuzika ndani ya kanisa lao,” alisema denti huyo.
Wanafunzi hao walieleza kuwa watumishi hao huwarubuni kwa kuwaeleza kuwa watawasaidia kuwasomesha iwapo watakuwa wakienda kwenye kanisa hilo na kuwaingilia.
Mzazi mmoja wa watoto hao, Julius, mkazi wa Kwamorombo alisema mtoto wake alimweleza kwamba amekuwa akifanyiwa mchezo mbaya na watumishi hao baada ya kupewa shilingi 2,000.
Alisema aligundua hilo kufuatia tabia ya mtoto wake kuchelewa kurudi nyumbani.
Mzazi mmoja wa watoto hao, Julius, mkazi wa Kwamorombo alisema mtoto wake alimweleza kwamba amekuwa akifanyiwa mchezo mbaya na watumishi hao baada ya kupewa shilingi 2,000.
Alisema aligundua hilo kufuatia tabia ya mtoto wake kuchelewa kurudi nyumbani.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema ambaye alifika hospitalini kuwajulia hali watoto hao alisikitishwa na kitendo hicho na kulitaka jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vipimo vya kidaktari ili kupata ukweli wa tukio hilo.
“Nimeongea na mkuu wa mkoa, Magesa Mulongo ambaye ameahidi kulifuatilia kwa kina suala hili na kujua undani wake,’’ alisema Lema.
Hata hivyo, watoto hao baadaye walihamishiwa katika Hospitali ya Seliani kwa ajili ya vipimo zaidi huku taarifa za awali zikithibitishwa na daktari wa hospitali hiyo kuwa, baadhi yao walikutwa na michubuko na kupanuka sehemu za siri hali inayooneshwa kuingiliwa.
Watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa kwa uchunguzi zaidi na Kamanda wa Polisi Arusha, Leberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
CREDIT:GPL