Vikosi vya uokoaji vikiwa eneo lilipoporomoka jengo hilo.
IDADI ya watu waliofariki dunia baada ya Kanisa la Mhubiri TB Joshua
kuporomoka nchini Nigeria hivi karibuni imefikia 115, huku 84 wakiwa
raia wa Afrika Kusini, 7 wa Nigeria na wengine waliobaki wakiwa bado
hawajafahamika wanatoka nchi gani.Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea Kanisa hilo la 'All Nations in Lagos' lililoporomoka siku 10 zilizopita.
Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Ndege iliyobeba majeruhi 25 wa ajali hiyo imewasili mjini Pretoria ambapo wataendelea kupata matibabu