Thursday, September 11, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA MTAMBO WA 10,000 WA BIOGAS KITAI

IMG_1607Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC Ndugu Elifariji Makongoro mara baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Kondo kilichoko katika kata ya Zinga wilayani Bagamoyo kushiriki katika siku ya kitaifa ya biogas iliyofanyika kijijini hapo na Mama Salma akiwa mgeni rasmi tarehe 10.9.2014.

IMG_1625Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea maonesho ya biogas yaliyofanyika katika Kijiji cha Kondo tarehe 10.9.2014. Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC  Ndugu Elifariji Makongoro (kulia) akimpatia maelezo mbalimbali ya kazi zinazofanywa na shirika hilo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza.
IMG_1631Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kijijini Kondo kwenye sherehe za kilele cha siku ya biogas kitaifa.
IMG_1648 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe huku akishirikiana na viongozi mbalimbali ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mtambo wa wa 10,000 wa Biogas hapa nchini. Mtambo huo unaomilikiwa na Ndugu Bakari Seif na Mkewe Mwanaidi Said (wa pili na wa tatu kutoka kushoto). Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndugu Eliakim Maswi, kulia kwa Mama Salma ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahizana. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kondo Ndugu Ramadhan Seleman akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC Ndugu Elifariji Makomgoro.
IMG_1660Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa CARMATEC  Ndugu Elifariji Makongoro kuhusu ujenzi wa mtambo huo na unavyofanya kazi.
IMG_1747Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na wageni waalikwa na mamia ya wananchi waqliohudhuria sherehe ya siku ya biogas kitaifa iliyofanyika katika Kijiji cha Kondo huko Bagamoyo tarehe 10.9.2014.