Saturday, July 19, 2014

HABARI ZA NAURA SPRING HOTEL KWAMBA INAWAKA MOTO SIO ZA KWELI PICHA ZILIKUWA NI ZAKUTENGENEZA

Zile habari ya kwamba hotel ya Naura Spring ya Arusha inawaka moto zilikuwa si za kweli ni watu wametengeza picha hizo ambazo zilikuwa zimeenea kwenye mitandao ya kijamii. Kamanda wa Polisi Arusha Liberatus Sabas ameongea jioni hii na vyombo vya habari na kukanusha habari za hotel hiyo ya kitalii jijini Arusha kwamba iliwaka moto hizo ni picha za kutengeneza hotel ipo salama kabisa kama unavyoona kwenye picha. Timu ya Vijimambo inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliotokea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas

Naura Spring Hotel inavyoonekana katika picha