Friday, March 7, 2014

VIDEO YA MWANAMUZIKI MWINGINE YAFUNGIWA MAISHA, INAONESHA MATUSI TUPU EBU JIONEE MWENYEWE...










Siku zinahesabika toka Wasanii watatu wa bongofleva ambao ni Snura, Jux na Dully Sykes kutangaza kwamba video zao za ‘nimevurugwa, uzuri wako na kabinti special’ zimepigwa stop kuonyeshwa kwenye TV za Tanzania kutokana na kuvuka mipaka ya kimaadili japo bodi ya filamu Tanzania imekanusha.
Mwenye huu wimbo hapa ni Mkenya,  anaitwa Blaqy ambae pamoja na video yake kupigwa marufuku kuonyeshwa kwenye TV nchini Kenya, kwa mujibu wa mitandao mbalimbali bado aliendelea kushikilia msimamo wake kwamba video hiyo haikua na tatizo lolote.
Alikaririwa kwenye barua aliyoiandika kwa bodi ya filamu Kenya kutaka kuifungulia hii video na kuacha kuzembea nafasi iliyopo kwa vijana kujitengenezea ajira nyingi kwenye kiwanda cha muziki.

Vyombo mbalimbali vya habari viliripoti kwamba Blaqy alisema hata hivyo huu wimbo haukupata nafasi kwenye media kwa sababu Watangazaji na Dj’s wameendekeza rushwa ya ngono na pesa.