Sunday, December 1, 2013

HIVI NDIVYO KHADIJA KOPA "MALKIA WA MIPASHO" ALIVYO VYAMIWA KARIAKOO......

MASKINI! Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omary Kopa amevamiwa na vijana wahuni wakitaka kumfanyia fujo kwa madai ya kukatiza mitaani akiwa ameongozana na ‘mwaume tata’.
Baadhi ya vijana wakiwa wamelizingira gari alilokuwemo Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa na mwanaume aliyedaiwa kuwa tata.
Tukio hilo lilijiri maeneo ya Kariakoo, Dar wiki iliyopita ambapo vijana hao walianza kwa kuzomea wakitaka kumshika mwanaume huyo waliyedai alikuwa amevaa nguo za jinsia ya kike.
Alichokifanya Khadija ni kuingia kwenye gari na kumwambia dereva aondoke haraka kukwepa kufanyiwa vurugu huku mwanaume huyo naye akiungana na malkia huyo kuondoka eneo hilo.
Vijana wakimzingira Khadija Kopa aliyekuwa ameambatana na 'mwanaume tata'.
Wakizungumza na gazeti hili, vijana hao walidai kuwa Khadija alijiabisha kwa kuongozana na mwanaume huyo.
Khadija aliliambia gazeti hili kuwa alishangazwa na tukio hilo lililomkuta na kusema kuwa mwanaume aliyeongozana naye ni mwimbaji mwenzake ambaye pia ni shemeji yake.
Alifunguka: “Hivi kuwa mwimba taarabu wa kiume ndiyo ushoga jamani? Au kuvaa kaptura ya kitenge ni tatizo? Mbona alikuwa amevaa mavazi mazuri tu ya kiume?”
...Vijana wakizidi kulizingira gari alilokuwemo Khadija Kopa.
Khadija alisema kuwa amewazoea mashabiki wake wa Kariakoo kwani huwa wakiwaona mastaa huwa na tabia hiyo na ndiyo maana walianza uzushi huku wakisema kuwa waimba taarabu wote ni wanawake, kitu ambacho si kweli.
“Sikuona sababu ya kuchukua hatua, nilikuwa najaribu kuwaelewesha lakini hawakunielewa, wakazidi kuzomea na kutuzingira ndiyo maana tuliamua kuondoka,” alisema Khadija.