Sunday, December 1, 2013

HII NDO AJALI ILIYO MUUA MSANII MAARUFU WA "FAST AND FURIOUS" PAUL WALKER MAPEMA LEO HUKO MAREKANI


Marekani. Mwigizaji wa Fast & Furious, Paul Walker amefariki dunia hivi punde nchini Marekani baada ya dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo kukosa ‘control’ na kugonga moja ya nguzo za taa za barabarani.

Nyota huyo wa kuigiza mwenye umri wa miaka 40 alikuwa abiria kwenye gariya kisasa na ajali hiyo ilitokea katika eneo la Santa Clarita.

Idara ya usalama ya nchini humo imedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kwamba watu wawili wamefariki dunia kwenye ajali hiyo.

Wawakilishi wa mwingizaji huyo wamethibitisha kwamba Paul Walker ni mmoja wa watu wawili waliofariki mchana wa LEO nchini Marekani.




“Ni kweli, tunapenda kuthibitisha kwamba mwigizaji Paul Walker  amefariki dunia leo katika ajali mbaya ya gari wakati alipokuwa akienda kuudhuria kuchangia mfuko wa  Reach Out Worldwide.



“Alikuwa abiria kwenye gari ya rafiki yake na wote wamepoteza maisha leo,” taarifa hizi zimesomeka kwenye akaunti maalum ya facebook ya muigizaji huyo