Kuhusu ukweli wa skendo hiyo, vyombo vya sheria vitazungumza lakini gazeti Uwazii limezungumza naye na hizi ni dondoo fupi za mazungumzo yao.
Kwa mujibu wa gazeti la Uwazi, denti huyo amekuwa akijulikana kama Felista, ila anatambulika pia kama Halima Hamad, hivi karibuni aliamua kujiita Leylat na wakati mwingine Leila.
Jina ambalo alijitambulisha kwa Kapuya ni Halima Hamad, upande mwingine hujitambulisha kama Halima Humudi, yaani huchezea ubini.
Gazeti hilo limeripoti kuwa, mwezi mmoja kabla ya sakata la Kapuya halijapamba moto, Felista alizungumza na waandishi wake wawili kwa nyakati tofauti, akielezea uhusiano wake na mheshimiwa huyo ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Miundombinu.
Felista alimweleza mwandishi wa kwanza ambaye ni mwanamke:“Nina stori kuhusu Kapuya, yule ni mtu wangu, ila subiri kidogo nitakupa stori kamili.”
Siku mbili baadaye, Felista alimfuata mwandishi wa pili ambaye ni wa kiume, akamwambia: “Kapuya ananitongoza, ngoja mambo yakae sawa nitakwambia.” Hata hivyo, waandishi hao waliamua kumpotezea.
Baada ya sakata hilo kuibuka kwa nguvu, kasi na ari, waandishi hao walimpigia simu Felista kumuuliza ilikuwaje akalifikisha suala mbali zaidi, huku akijisema yeye ni mwanafunzi wakati siyo kweli?
Felista alimjibu mwandishi wa kwanza: “Huyo aliyepeleka hizo habari ni Leylat. Mimi Kapuya nafahamiana naye kwa sababu nilishiriki vikao vya usuluhishi kati ya Leylat na Kapuya. Walimalizana vizuri. Mimi kama shahidi nilipata shilingi 3,000,000.
“Siku ya kwanza nilipewa shilingi 2,300,000, baadaye alinimalizia shilingi 700,000, tukawa tumemalizana.”
Msichana huyo, alidai yeye ni yatima, akiishi kwa tabu sana, Mama Salma akaingia mkenge na kumpa kiwanja Mbagala. Baadaye ilipokuja kujulikana, alishtakiwa kwa utapeli, akapelekwa mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam.
Felista alikiri kuwekwa Segerea kisha akajitetea: “Kuna watu walitaka kunigombanisha na Mama Salma lakini mbona nilitoka?”
Felista, alishawahi kumuibia marehemu Steven Kanumba kamera, alipokwenda ofisini kwake, akijidai ni yatima na ana kipaji cha kuigiza, alipopata mwanya tu, alimliza supastaa huyo ambaye alifariki dunia, Aprili 7, mwaka jana.
Ukiachana na hilo la Kimei ambalo limetajwa na Kapuya, yapo matukio mengine ambayo Felista alishayafanya, ikiwemo kudanganya anasoma alipiwe ada, vitabu, madaftari na sare za shule, kumbe ni ‘gia’ yake ya kupata fedha kwa njia ya udanganyifu.
Uchunguzi wa gazeti hilo unalo jawabu kuwa kama kuna uongo ambao jamii haipaswi kubisa kukubaliana nao ni huu kwamba Felista ana umri wa miaka 16 na anasoma sekondari.
Gazeti hilo limebaini kuwa Felista ni mama wa mtoto mmoja na lilipombana alikiri: “Ni kweli nina mtoto mmoja, nina umri wa miaka 21
Kwa mujibu wa gazeti la Uwazi, denti huyo amekuwa akijulikana kama Felista, ila anatambulika pia kama Halima Hamad, hivi karibuni aliamua kujiita Leylat na wakati mwingine Leila.
Jina ambalo alijitambulisha kwa Kapuya ni Halima Hamad, upande mwingine hujitambulisha kama Halima Humudi, yaani huchezea ubini.
Gazeti hilo limeripoti kuwa, mwezi mmoja kabla ya sakata la Kapuya halijapamba moto, Felista alizungumza na waandishi wake wawili kwa nyakati tofauti, akielezea uhusiano wake na mheshimiwa huyo ambaye kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Miundombinu.
Felista alimweleza mwandishi wa kwanza ambaye ni mwanamke:“Nina stori kuhusu Kapuya, yule ni mtu wangu, ila subiri kidogo nitakupa stori kamili.”
Siku mbili baadaye, Felista alimfuata mwandishi wa pili ambaye ni wa kiume, akamwambia: “Kapuya ananitongoza, ngoja mambo yakae sawa nitakwambia.” Hata hivyo, waandishi hao waliamua kumpotezea.
Baada ya sakata hilo kuibuka kwa nguvu, kasi na ari, waandishi hao walimpigia simu Felista kumuuliza ilikuwaje akalifikisha suala mbali zaidi, huku akijisema yeye ni mwanafunzi wakati siyo kweli?
Felista alimjibu mwandishi wa kwanza: “Huyo aliyepeleka hizo habari ni Leylat. Mimi Kapuya nafahamiana naye kwa sababu nilishiriki vikao vya usuluhishi kati ya Leylat na Kapuya. Walimalizana vizuri. Mimi kama shahidi nilipata shilingi 3,000,000.
“Siku ya kwanza nilipewa shilingi 2,300,000, baadaye alinimalizia shilingi 700,000, tukawa tumemalizana.”
Mwandishi wa pili alipomuuliza, alijibu: “Jamani siyo mimi, yule ni Leila. Yule mtoto sijui kafikishaje hayo mambo huko, ila mimi najua kila kitu.”
Historia ya huyu binti kwa mujibu wa gazeti la Uwazi:
Felista wa Kapuya ndiye yule binti aliyewahi kumtapeli mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma kupitia Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama). Msichana huyo, alidai yeye ni yatima, akiishi kwa tabu sana, Mama Salma akaingia mkenge na kumpa kiwanja Mbagala. Baadaye ilipokuja kujulikana, alishtakiwa kwa utapeli, akapelekwa mahabusu kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam.