Kikizungumza na Ijumaa Wikienda chanzo chetu kilicho makini, kilisema kinawashangaa sana Wastara na mwenzi wake huyo kuukana upenzi wao kila kukicha wakati picha zinajieleza.
“Wastara amekuwa akimkana Bond kuwa si mpenzi wake ila ni kaka yake sasa hebu tazama picha zao mpya, hata mtoto mdogo humdanganyi kitu,” kilisema chanzo hicho huku wawili hao wakiendelea kukanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi.