Kwa mujibu wa meneja wa Wema, Martin Kadinda, Jokate aliibuka Jumanne iliyopita usiku kwenye msiba wa baba Wema uliochukua nafasi nyumbani kwao Sinza-Mori jijini Dar na kumfariji hadi usiku mnene.
Jokate Mwegelo.
“Fani ya urembo na ubunifu ni fani za watu makini sana ambao chuki
kwao ni mwiko, nimefurahishwa na kitendo cha Jokate kuja msibani kwani
anaonyesha dhahiri kuwa ni mtu mwenye huruma na imani,” alisema Kadinda.