Monday, November 4, 2013

JOHN SHIBUDA AZUILIWA KUHUDHURIA KIKAO CHA CHADEMA KWA MADAI KUWA YEYE NI KIBARAKA WA CCM.


Kikao kinachojadili maendeleo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya ziwa Mashariki (Mara,Simiyu na Shinyanga) jana  jioni   kimemtimua Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda baada ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
 
Shibuda ambaye alihudhuria kikao hicho kama mbunge wa Kanda hiyo alijikuta akipatwa na zahama hiyo baada ya mjumbe mmoja kutoa hoja kwa Mwenyekiti wa Kikao hicho kwamba Shibuda atoke nje.
 
Mjumbe huyo alisema Shibuda ni mamluki na kibaraka wa CCM hasa kutokana na matamshi yake kadhaa dhidi ya Chadema na mwenendo wake usioridhisha ndani ya chama.Aliongeza kwamba Shibuda alikuwa kwenye kikao hicho kwa lengo maalum la kukusanya habari na kupeleka CCM.
 
Hatimaye hoja ya mjumbe huyo iliungwa mkono na wajumbe wote na hatimaye ikapigwa kura ya kutokuwa na imani naye. Shibuda alikubali kuondoka ndani ya kikao hicho na  kuwaachia  kikao  chao