Tuesday, November 12, 2013

GARI KATIKA MSAFARA WA RAIS LILIVYOPATA AJALI GEITA......

Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
Askari akilikagua gari.
Mwandishi Peter Makunga akiwa anaendelea kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo, hospitali ya wilaya ya Geita.
Msafara wa Rais  wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete mkoani Geita, Siku ya jana umeingia dosari baada ya gari moja lilokuwa kwenye msafara huo kupinduka na kujeruhi watu watano.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Geita  Lenard  Paul ajali hiyo ilitokea saa 3 na dakika 45 asubuhi siku ya jana katika eneo la Nyankumbu kilomita 3 kutoka makao makuu ya mkoa wa geita.
Kamanda Paulo amesema gari aina ya Toyota Landcruzer yenye namba DFP9730 lililokuwa likiendeshwa Yungi Mkwati, mali ya Bohari kuu ya Madawa (MSD), lilipinduka baada ya kuteleza kwenye lami iliyomwagwa barabarani.
Amewataja Waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni mwandishi Peter Makunga wa Radio Kahama Fm na Radio Free Afrika, Peter Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda Moderator wa Tovuti ya mabadiliko.com, meneja wa MSD kanda ya Ziwa Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yungi Mkwati.