Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake. |
Nyawana amefariki akiwa kwake maeneo ya Mwananyamala B na mwili wake sasa umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala, Dar.
Marehemu Nyawana alizaliwa mwaka 1977 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupata elimu yake katika shule mbalimbali kuanzia Msingi, Sekondari na elimu ya juu.
Shule ya Msingi Zanaki ndipo alipopata elimu yake mwaka 1983 na kuhitimu mwaka 1989, wakati ile ya Sekondari alisoma Masjid Quba mwaka 1992 na kumalizia Al Haramain.
Baada ya hapo alisomea Uhadhiri kabla ya kumaliza na kusomea masomo ya Uandishi wa Habari na Utangazaji, ambapo pia alishiriki shindano la urembo na kunyakua taji la Miss Tabora, mwaka 1996.
Mbali na sanaa ya uimbaji, pia Nyawana ni mwandishi na mtangazaji, aliyefanya vyema mno, hasa kwa kutangaza vipindi vya taarabu, katika redio kadhaa, ikiwamo ile ya Voice of Tabora.
Baadhi ya nyimbo alizorekodi marehemu ni pamoja na 'Nipo Kamili Nimejipanga' na 'Umesharoga Wangapi', nyimbo ambazo zilitangaza na kuonyesha kipaji chake halisi.
Baadhi ya makundi ya taarab aliyowahi kufanya nayo kazi marehemu ni, Kings Modern Taarab na Tanzania Moto Modern Taarab, maarufu kama T-Moto.
Mungu ailaze mahali pema peponi! AMEN!