MWANADADA anayeendesha maisha yake kwa kuuza nyago kwenye filamu Bongo, Wastara Juma ameumia mguu baada ya kuwekewa mwingine mpya wa bandia huko Nairobi nchini Kenya.
“Nimeshindwa kula sikukuu mbali na watoto wangu ndiyo maana nikaja mara moja japokuwa siko vizuri kwa sababu niliumia kwenye mazoezi ya kutumia mguu mpya huko Nairobi na sasa nauguza kidonda lakini baada ya hapo nitarudi tena Nairobi kwa ajili ya matibabu,” alisema Wastara.