Sunday, October 27, 2013

UPDATES:MBUNGE WA CCM "EZEKIEL MAIGE" ATUHUHUMIWA KUTOA RUSHWA YA SH.MIL 50 KUWASHAWISHI MADIWANI....

Mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige (CCM) anadaiwa kutoa rushwa ya Shilingi milioni 50 kwa lengo la kushawishi madiwani wahamishe Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala katika Kata ya Busangi kwenda Segese.

Kwamba, madai hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mibako Mabubu wakati akiwajibu waandishi wa habari, kutokana na tuhuma za baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Msalala kupewa rushwa: “Ninyi waandishi wa
habari mmeona hayo ndio ya kuandika, mbona hamuandiki kuhusu Mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige kutoa Sh milioni 50 kwa ajili ya kushawishi madiwani wahamishie Makao makuu ya Halmashauri ya Msalala?” alihoji Mabubu.

Maige alipotafutwa na waandishi wa habari kuzungumzia tuhuma hizo, alisema kuwa kata hizo zote zipo katika jimbo lake, kwani kufanya hivyo haoni mantiki yoyote kwa sababu maeneo yote ni yake.  Maige akasema kuwa kuna baadhi ya Madiwani wamepanga kumchonganisha na wapigakura wake na kama yeye ametoa Sh milioni 50, basi ajitokeaze diwani athibitishe kama kweli amewapa