Mahakama
nchini Malaysia, imeamua kuwa watu wasio waisilamu wasitumie jina
'Allah' kumaanisha Mungu katika katika imani zao na kubatilisha uamuzi
wa mahakama ndogo uliotolewa mwaka 2009.
Mahakama
ya rufaa ilisema kuwa jina Allah linapaswa tu kutumiwa na waumini wa
kiisilamu la sivyo linaweza kuzua taharuki miongoni mwa jamii.
Wakristo
wanateta kuwa wamekuwa wakitumia jina hilo la Allah katika lugha ya
Malay na ambalo lilitokana na lugha ya kiarabu kumaanisha Mungu kwa
miaka mingi na kuwa uamuzi wa mahakama unakiuka haki zao.Watu wa imani
zote nchini Malaysia wanatumia neno Allah kumaanisha Mungu.
Mwanamke mmoja mkristo alisema kuwa uamuzi huo utaathiri jamii pakubwa.
"ikiwa
tutawazuia watu wengine kutumia jila la Allah, basi itatubidi kutafsiri
Bibilia nzima upya" Ester Moiji kutoka jimbo la Sabah aliambia BBC.
Umauzi
ulitolewa na mahakama ndogo mwaka 2009 ulisababisha taharuki baina ya
waisilamu na wakristo huku makanisa na misikiti ikishambuliwa.
Ilitokea
baada ya serikali kusema kuwa jarida la kikatoliki la The Herald,
haliwezi kutumia jina Allah katika makala yake ya lugha ya Malay
kumaanisha Mungu kwa kikristo.
Wahariri
wa jarida hilo lilikwenda mahakani kupinga uamuzi huo na mahakama
ikafanya uamuzi uliowapendelea. Serikali baadaye ilikata rufaa.
Lakini
katika uamuzi wake leo, jaji alisema kuwa jina Allah haliwezi kutumika
kwa dini ya kikrsito kumaanisha Mungu na kuwa ikiwa jina hilo litatumiwa
basi huenda likazusha taharuki baina ya jamii.
Mhariri wa jarida hilo alisema kuwa alighadhabishwa na kushangazwa sana na uamuzi wa mahakama na kwamba atakata rufaa.
Wafuasi
wa jarida hilo wamesema kuwa Bibilia zilizoandikwa kwa lugha ya Malay
zimekuwa zikimtaja Allah kumaanisha Mungu kwa kikristo tangu zamani san