Tuesday, September 3, 2013

WATANZANIA WENGI BADO NI MASKINI WA KUTUPWA"..........PINDA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema licha ya kuwapo kwa mipango mingi ya serikali, lakini Watanzania wengi bado hawajaondokana na umaskini.

Hata hivyo, Pinda amesema serikali imebaini kuwapo kwa kasoro nyingi katika utekelezaji wa mipango mingi ya maendeleo na kuanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Mizengo%20Pinda(1).jpg

Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Mpango wa Maendeleo ya Binadamu Tanzania (HDR) mjini Dodoma jana.

 Hotuba ya Waziri Mkuu Pinda, alisomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.

Alisema uzinduzi wa HDR utaisadia juhudi za serikali katika ufuatiliaji wa maendeleo kwa wananchi wake na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo.

Aidha, alisema uzinduzi huo utaibua mambo mengi mapya katika kufikia maendeleo ya watu.
Akichangia wakati wa uzinduzi huo wa HDR,  Mbunge Injinia Stella Manyanya (CCM-Viti Maalum), alisema watu wengi hupenda kuitwa maskini kwa lengo la kupata misaada badala ya kujiletea maendeleo chanya.

Naye Mbunge Susan Kiwanga (Viti Maalum- Chadema), aliitaka serikali kugawa rasilimali za nchi kwa