Katibu wa IPC Francis Godwin akiongoza maandamano ya wanahabari na wadau huku akiwa juu ya gari na picha ya marehemu Daud Mwangosi.
Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari mkoa wa Iringa ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi yakipita eneo ya Uhindini.
Wanahabari Iringa katika maandamano ya kumuenzi marehemu Mwangosi jana.
Wanahabari wa vyombo mbalimbali na wadau wa habari mkoa wa Iringa wakiwa katika maandamano ya amani ya kumuenzi aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC).
Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari yakipita eneo la soko kuu la manispaa ya Iringa.
Wananchi wakishuhudia maandamano hayo.
Katibu Mtendaji wa IPC, Francis Godwin akitoa taarifa ya kuanza kwa maandamano ya kumuenzi marehemu Daud Mwangosi jana.
Katibu wa IPC Francis Godwin (kushoto) akikabidhi picha ya marehemu Daud Mwangosi kwa Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard (kulia), wanaoshuhudia ni Mzee Fulgence Malangalila na Majid Mjengwa.
Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard kushoto akikabidhi picha ya Mwangosi kwa mwasisi wa IPC, Mzee Fulgence Malangalila.
MAANDAMANO ya wanahabari mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) na mwandishi wa Channel Ten, Marehemu Daud Mwangosi yatikisa mji wa Iringa jana.
Maandamano hayo yalianza saa 4 asubuhi katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa yakipita katika maeneo mbalimbali ya mji wa Iringa kabla ya kupokelewa na mwenyekiti wa IPC, Frank Leonard katika ukumbi wa maktaba ya mkoa kwa mkutano wa wadau wa habari.