![](https://fbcdn-sphotos-b-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash4/1240007_194533030726342_1497150044_n.jpg)
Msanii makali wa bongo fleva Sam wa ukweli leo katika kipindi cha leo
tena amewatia watu simanzi kutoka na historia ya maisha yake ambayo
imejaa majonzi na simanzi.
Akizungumza na Dina katika kipindi cha leo tena katika redio ya clouds sam amesema kuwa katika maisha yake hatasau maisha magumu sana aliyopitia wakati akiwa mtoto hadi kuwa sam wa ukweli,Amesema kuwa baba yake mzazi aliwahi kupotea na na kufanya watu kuamini kuwa alifariki jambo lililofanya waishi maisha magumu sana huku wakitegemea maisha ya kilimo na baada ya muda ikabidi mama yake sam aolewe na mwanaume mwingine.

![]() |
Sam wa ukweli katika pozi |
Sam anasema kuwa baada ya hapo baba huyo wa kufikia alisema sam kamuua mwanae maksudi na kuleta mtafaruku mzito katika familia yao jambo lililosababisha ndoa hiyo kuvunjika na wakarudi kwa bibi yake mzaa mama na ndipo walipokuja kushangaa baada ya baba yao mzazi ambae waliambiwa kafa kurudi nyumbani akiwa mzima kabisa na ndio safari ya kuja dar kwa mara ya kwanza