Sunday, September 1, 2013

MAJAMBAZI.. YAPORA PESA NA KUJERUHI AFRIKANA JIJINI DAR..



 
Kundi la majambazi waliokuwa na silaha za moto wakiwa na magari mawili Landcruiser na Noah wamevamia kampuni inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa fenicha ya Diab Furniture Manufacturing Company iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam. Majambazi hayo baada ya 
kuvamia eneo hilo yalifanikiwa kupora sefu iliyokuwa na fedha pamoja na kuwajeruhi mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo na mlinzi.
(Pichani juu: Difenda la Polisi likiondoka eneo la tukio na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo aliyejeruhiwa)