Sunday, September 1, 2013

DIAMOND AFUNGUKA KUTENGENEZA NUMBER ONE AFRIKA KUSINI

Diamond Platnumz akiandaa video yake mpya ya Number One nchini Afrika Kusini.
Diamond akipozi katika kamera wakati akiandaa video ya Number One.
Akielezea kwa nini ameamua kufanya video yake hiyo nchini Afrika Kusini.
Msanii Mahiri wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amefunguka na kuelezea sababu za kuamua kufanya video ya ngoma yake mpya ya Number One nchini Afrika Kusini. Diamond aliyetumia kiasi cha Dola za Kimarekani 30,000 zaidi ya shilingi milioni 48 za Kitanzania kutengeneza video hiyo, ameeleza hayo katika video aliyoiweka kwenye Blog yake inayoonyesha maandalizi ya utengenezaji wake. Diamond anasemaa ameamua kuifanyia nchini Afrika Kusini ili kuwa na kitu tofauti, kupata mandhari, washiriki na radha tofauti. ANGALIA BEHIND THE SCENE NA DIAMOND MWENYEWE AKIELEZEA KUHUSU VIDEO YA NUMBER ONE HAPA CHINI: