Saturday, September 28, 2013

UPDATES:MATEKA WA WESTGATE WATOBOLEWA MACHO, WANG'OLEWA PUA NA KUNYOFOLEWA VIDOLE KWA KOLEO..

Askari wamesimulia mateso makali ya kutisha yaliyofanywa na magaidi kwenye jengo la Westgate mjini Nairobi juzi wakidai kuwa mateka walikatwa viungo, macho yao kutobolewa na kutelekezwa wakiwa wamening'inizwa katika vishikizo darini. 

Watu hao walisemekana kuhanisiwa na vidole vyao kunyofolewa kwa kutumia koleo kabla ya kupofolewa macho na kunyongwa.

Watoto walikutwa wakiwa wamekufa ndani ya majokofu ya kuhifadhia chakula huku visu vikiwa bado vimeng'ang'ania kwenye miili yao, imedaiwa.

Wengi wa magaidi hao walioshindwa mapigano, hatahivyo, waliripotiwa kupatikana wakiwa 'wameteketea moto na kubaki majivu', kuchomwa moto na mwenye msimamo mkali wa mwisho kujaribu kuficha utambulisho wao.

Taarifa hizo za kutisha zimekuja juzi huku picha za kwanza zikiibuka kutoka ndani ya jengo hilo lililobomoka, zikionesha rundo la miili ikiwa imetelekezwa kila kona sakafuni.

Sehemu kubwa ya jengo hilo iliangamizwa katika mapigano kati ya magaidi na vikosi vya Kenya.

Ikiwa imelala kwenye kifusi inahofiwa kuwa miili ya wananchi wengi wanaofikia 71 ambao wamethibitishwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya kwamba walikuwa hawajulikani waliko.

Pamoja na wapelelezi, wakiwamo FBI na Metropolitan Police, bado haikuwezekana kufikia sehemu iliyobomoka ya jengo hilo kwa hofu ya kulipuka mabomu, inaweza kuchukua hadi wiki kujua kwa uhakika nani bado yuko ndani ya jengo.

Juzi, askari na madaktari ambao walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuingia ndani ya jengo hilo baada ya kuwa imedaiwa Jumanne, walizungumzia matukio ya kutisha ndani.

"Unakuta watu wakiwa na vishikizo wakining'inia kutoka kwenye dari," alisema mmoja wa madaktari wa Kenya, ambaye hakutaka kutajwa jina.

"Walinyofolewa macho, masikio na pua. Wanachukua mkono wako na kuuchonga kama penseli kisha wanakwambia uandike jina lako kwa kutumia damu. Walicharanga visu ndani ya mwili wa mtoto mmoja.

"Hakika kama unaangalia miili yote, isipokuwa wote waliotoroka, vidole vimekatwa kwa koleo, pua zimenyofolewa kwa koleo. Hapa ilikuwa maumivu."

Askari mmoja, ambaye alipiga picha kaunta ta mikate na katika ArtCaffe, alisema alishikwa ganzi kwa kile alichokiona hivyo anahitaji ushauri nasaha.

Wataalamu wa kutegua mabomu wakiwa na mbwa wa kutambua mabomu juzi walikuwa wakikagua sehemu ya jengo hilo ambayo inahofiwa kuwa na mabomu kabla ya kuruhusu maofisa wa mahakama, polisi na vikosi kusaka miili.

Picha pia zilizoibuka juzi zimebainisha ukweli wa kiwango cha uharibifu uliosababishwa katikati wakati wa mapambano hayo ya siku nne kati ya vikosi vya Kenya na wanamgambo wa Kiislamu.

Picha za kwanza zilizopigwa ndani ya eneo hilo zinaonesha shimo kubwa katika paa la jengo hilo baada ya ghorofa tatu kuanguka pale askari wa Kenya walipolipua bomu ndani ya jengo, kuweza kupata nafasi ya kuwasaidia waathirika, ofisa wa serikali alisema.

Kubomoka huko kulitokea Jumatatu pale vikosi vya serikali vilipofanya shambulio kubwa katika jengo hilo ambako watu wanaofikia 150 wanahofiwa kuwa wameuawa.

Wakati wa kupambana na moto, mateka waliripotiwa kuchinjwa kuanzia sikio moja hadi jingine na walitupwa wakipiga mayowe kutoka kibaraza cha ghorofa ya tatu huku utekaji huo ukielekea kufika mwisho. Timu za mahakama bado zinahangaika katikati ya milima ya vifusi, huku wakihofu miili mingine zaidi bado haijapatikana.

Askari wa Kenya akijipanga namna ya kutoka...


Ghorofa ya juu ya Westgate Mall baada ya kupigwa kombora na vikosi vya Kenya...
Ghorofa tatu zilizobomolewa kwa kombora...
Uharibifu mkubwa baada ya ghorofa kulipuliwa kwa kombora...

Baadhi ya magari baada ya kuteketea kwa moto juu ya jengo la Westgate Mall...
Sehemu ya maegesho ya magari ndani ya jengo hilo baada ya kupigwa kombira...
Mwili wa mmoja wa waathirika ukiwa umetelekezwa ndani ya jengo hilo.