KAKA wa staa wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Juma Juma
ameliambia Risasi Mchanganyiko kwamba dada yake hatafunga tena ndoa
nyingine hapa nchini.
“Iwapo dada yangu akitaka kuolewa atafanya hivyo Uarabuni siyo hapa
kabisa,” alisema kaka huyo na kudai kuwa ameshuhudia mateso mengi ya
dada yake kwa wanaume wa Kitanzania.
Kaka huyo amesisitiza kwamba wanaume wasipate tabu ya kumuuliza dada yake kuhusu suala la ndoa kwani watajisumbua bure.
Juma alizungumza kwa niaba ya dada yake ambaye awali alipigiwa simu ili
kuulizwa kama alikuwa na mpango wa kufunga ndoa nyingine hapa nchini.
Hata
hivyo, Wastara alimwachia kaka yake huyo kujibu badala yake, ingawaje
kaka huyo hakufafanua kama dada yake ameshapata mtu wa kufunga naye ndoa
huko Uarabuni.
Wastara alifunga ndoa tatu na wanaume tofauti na mume wake wa mwisho
alikuwa msanii wa filamu, Juma Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia
mapema mwaka huu.
SOURCE:GPL