Thursday, August 29, 2013

POLISI WATOA ZAWADI YA SHILLINGI MILLIONI 100!! BAADA YA KIPIGO CHA MAJAMBAZI LEO!


Kufuatia tukio la wizi lililotokea leo katika benki ya Habib African iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuibiwa zaidi ya shilingi milioni 900 za Tanzania, Jeshi la Polisi limetangaza dau la shilingi milioni moja kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa majambazi yaliyofanya hicho kitendo. Majambazi hayo yaliyokuwa yamevaa sare za Jeshi la Polisi yalivamia benki hiyo na kupora Dola za Kimarekani 181,885 sawa na shilingi milioni 293.9 za Tanzania. Pia yalipora jumla ya shilingi milioni 700 za Tanzania na kufanya jumla ya fedha zilizoibiwa kuwa shilingi milioni 993.9.