Friday, August 30, 2013

UPDATES:FRANK RIBERY NDIYE MCHEZAJI BORA WA ULAYA 2012-2013

Franck Ribéry akiwa na tuzo yake.
MCHEZAJI wa Bayern Munich, Franck Ribéry ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2012 - 2013. Ribéry amewabwaga wachezaji Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa kupanga makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) kwa msimu huu. Msimu uliopita, Ribéry aliiongoza timu yake ya Bayern Munich kuchomoza na ushindi katika fainali dhidi ya Borussia Dortmund kwenye Uwanja wa Wembley uliopo London, England. Msimu wa 2011/14 tuzo hiyo ilikwenda kwa kiungo wa Barcelona, Andrés Iniesta