Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Mohamed Azzan.
Wakati Jeshi la Polisi Tanzania
likiweka bayana kwamba, linamchunguza Mbunge wa Kinondoni kwa ‘leseni’
ya CCM, Mheshimiwa Idd Mohamed Azzan kama kweli anajihusisha na biashara
ya madawa ya kulevya, baadhi ya wapiga kura wake wameibuka na kuthubutu
kusema kiongozi huyo hauzi unga.
Wakizungumza juzi Bamaga, Mwenge
jijini Dar, wapiga kura hao kutokea CCM, walisema madai kwamba mbunge
wao ni mfanyabiashara wa ‘unga’ yamewashangaza sana.Walisema
haiingii akilini hata kidogo kwa mtu ambaye amepata utajiri wake huku
majirani wakimuona halafu aangushiwe kashfa ya kufanya biashara hiyo
haramu.
“Sisi hapa (Magomeni Makanya) tunamjua
Idd tangu zamani akiwa kijana mdogo. Alikuwa na teksi akiwa anaendesha
mwenyewe, akaja akanunua ya pili.Na GPL
“Mwaka 1986 aliziuza, akanunua
daladala aina ya Costa, akawa anaendesha mwenyewe, tena ilikuwa inafanya
safari za Pugu Kariakoo, akaja akanunua lori, akawa anaendesha
mwenyewe,” alisema mzee Mussa, mkazi wa eneo hilo.
Naye Bakari au maarufu kwa jina la
Jabu, alisema yeye anakumbuka mwaka 1986, mheshimiwa akiwa anasaka
maisha alifanya biashara ya kupeleka redio Bujumbura nchini Burundi
kisha anarudi na mashati yalikuwa maarufu kwa jina la Juliana, anauza
Dar, tayari kipindi hicho Idd ana fedha zake.
“Sasa leo wanapozuka watu na kusema
anauza dawa za kulevya, tunashangaa sana. Sisi majirani zake achilia
mbali kuwa wapiga kura wake tungejua.
“Watu wanaojazana nyumbani kwake kabla
hajaamua kuikarabati hii nyumba hapa wengi ni wale wenye matatizo,
wanaomba msaada,” alisema mzee huyo.
Mzee mwingine, Hussein alisema
anakumbuka mwaka 1989, yeye alikuwa shahidi wakati Azzan alipokopeshwa
semi trela aina ya Mercedes Benz na kaka yake kwa makubaliano ya kumlipa
fedha mwaka 1992.
“Azzan alikubali masharti hayo, akawa
anaendesha mwenyewe kwenda nje ya nchi. Alikuwa akienda Rwanda, Burundi,
Zambia, Malawi mpaka Kongo.
“Na alikuwa akirudi anatubebea zawadi za
chakula wazee wake kwa sababu ya ukaribu, mwaka elfu moja mia tisa na
tisini na mbili alilipa deni, semi trela ikawa yake na akanunua jingine
kama hilo.
“Nakumbuka kuna mwaka alipata ajali mbaya sana kule Ngara, akaumia na kulazwa, tukapata taarifa.
“Alipotoka akaamua kuanzisha Kampuni ya
Azzan Investment na kununua mabasi mengi ya kukodisha, ndivyo ninavyojua
mimi asili ya utajiri wa huyu bwana. Azzan hauzi unga bwana,” alisema
mzee huyo.
Siku hiyohiyo, Uwazi lilimtafuta kwa
simu Mheshimiwa Azzan na kumuuliza kama anawajua wazee hao ambapo
alisema ni wazee wake anaowaheshimu sana, lakini akaomba asiongee kwa
undani sana kwa vile alikuwa kikaoni.
Hivi karibuni, mtu mmoja aliyedai yupo
jela Hong Kong, China kwa ishu ya unga aliandika majina ya watu aliodai
ndiyo wafanyabiashara wa madawa ya kulevya na kuyatumbukiza majina hayo
mtandaoni. Miongoni mwa majina hayo limo la Idd Azzan.Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Mohamed Azzan. Na Mwandishi Wetu
WAKATI Jeshi la Polisi Tanzania likiweka
bayana kwamba, linamchunguza Mbunge wa Kinondoni kwa ‘leseni’ ya CCM,
Mheshimiwa Idd Mohamed Azzan kama kweli anajihusisha na biashara ya
madawa ya kulevya, baadhi ya wapiga kura wake wameibuka na kuthubutu
kusema kiongozi huyo hauzi unga.
Wakizungumza na Uwazi juzi Bamaga,
Mwenge jijini Dar, wapiga kura hao kutokea CCM, walisema madai kwamba
mbunge wao ni mfanyabiashara wa ‘unga’ yamewashangaza sana.
Walisema haiingii akilini hata kidogo
kwa mtu ambaye amepata utajiri wake huku majirani wakimuona halafu
aangushiwe kashfa ya kufanya biashara hiyo haramu.
“Sisi hapa (Magomeni Makanya) tunamjua
Idd tangu zamani akiwa kijana mdogo. Alikuwa na teksi akiwa anaendesha
mwenyewe, akaja akanunua ya pili.
“Mwaka 1986 aliziuza, akanunua daladala
aina ya Costa, akawa anaendesha mwenyewe, tena ilikuwa inafanya safari
za Pugu Kariakoo, akaja akanunua lori, akawa anaendesha mwenyewe,”
alisema mzee Mussa, mkazi wa eneo hilo.
Naye Bakari au maarufu kwa jina la Jabu,
alisema yeye anakumbuka mwaka 1986, mheshimiwa akiwa anasaka maisha
alifanya biashara ya kupeleka redio Bujumbura nchini Burundi kisha
anarudi na mashati yalikuwa maarufu kwa jina la Juliana, anauza Dar,
tayari kipindi hicho Idd ana fedha zake.
“Sasa leo wanapozuka watu na kusema
anauza dawa za kulevya, tunashangaa sana. Sisi majirani zake achilia
mbali kuwa wapiga kura wake tungejua.
“Watu wanaojazana nyumbani kwake kabla
hajaamua kuikarabati hii nyumba hapa wengi ni wale wenye matatizo,
wanaomba msaada,” alisema mzee huyo.
Mzee mwingine, Hussein alisema
anakumbuka mwaka 1989, yeye alikuwa shahidi wakati Azzan alipokopeshwa
semi trela aina ya Mercedes Benz na kaka yake kwa makubaliano ya kumlipa
fedha mwaka 1992.
“Azzan alikubali masharti hayo, akawa
anaendesha mwenyewe kwenda nje ya nchi. Alikuwa akienda Rwanda, Burundi,
Zambia, Malawi mpaka Kongo.
“Na alikuwa akirudi anatubebea zawadi za
chakula wazee wake kwa sababu ya ukaribu, mwaka elfu moja mia tisa na
tisini na mbili alilipa deni, semi trela ikawa yake na akanunua jingine
kama hilo.
“Nakumbuka kuna mwaka alipata ajali mbaya sana kule Ngara, akaumia na kulazwa, tukapata taarifa.
“Alipotoka akaamua kuanzisha Kampuni ya
Azzan Investment na kununua mabasi mengi ya kukodisha, ndivyo ninavyojua
mimi asili ya utajiri wa huyu bwana. Azzan hauzi unga bwana,” alisema
mzee huyo.
Siku hiyohiyo, Uwazi lilimtafuta kwa
simu Mheshimiwa Azzan na kumuuliza kama anawajua wazee hao ambapo
alisema ni wazee wake anaowaheshimu sana, lakini akaomba asiongee kwa
undani sana kwa vile alikuwa kikaoni.
Hivi karibuni, mtu mmoja aliyedai yupo
jela Hong Kong, China kwa ishu ya unga aliandika majina ya watu aliodai
ndiyo wafanyabiashara wa madawa ya kulevya na kuyatumbukiza majina hayo
mtandaoni. Miongoni mwa majina hayo limo la Idd Azzan.