Amatus Joackim Liyumba.
Hamida Hassan na Gladness Mallya
MNAMKUMBUKA aliyekuwa kigogo
wa Benki Kuu ya Tanzania aliyefungwa jela miaka miwili kwa makosa ya
matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa mali za umma, Amatus Joackim
Liyumba? Basi amekwaa balaa jipya, Uwazi linajua kila kitu.
Liyumba
na mwanamke aliyedai ni mke wake, Aurelia Paulo Ngowi wamefikishana
Mahakama ya Kinondoni, Dar kisa kikidaiwa ni mzee huyo kumtaka mwanamke
huyo kuondoka haraka kwenye nyumba anayoishi na watoto wao wawili.
Nyumba
hiyo ipo Mbezi ya Afrikana, jijini Dar. Mbali na kuwa makazi, lakini
sehemu ya mbele ya nyumba hiyo ni Hoteli Amjen yenye kupata wateja kila
siku.
Jina
la Amjen linadaiwa ni muuganiko wa majina ya Amatus na Jennifer ambaye
ni mtoto mmoja kati ya hao wawili wa mzee huyo. Na GPL
Aurelia ndiye aliyekimbilia
mahakamani kuomba msaada ambapo shauri lake lilifunguliwa kwa namba 59,
2013 mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina moja
la Rugemalira.
Baada ya
ombi hilo, mahakama ilimwamuru Liyumba kumwacha mkewe na watoto hao
waendelee kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka shauri hilo litakapotatuliwa
kisheria.
Haikujulikana mara moja kama Liyumba anataka mkewe na watoto waondoke kwenye nyumba hiyo na yeye kwa sasa anaishi wapi.
Jitihada za kumtafuta zilifanyika, simu yake ya mkononi haikuwa hewani huku ikidaiwa kwamba namba husika haitumii tena.
Baadhi ya
watu wake wa karibu waliliambia Uwazi kwamba, kwa sasa Liyumba anaishi
Kinondoni, Dar es Salaam lakini kupatikana kwenye simu ni ishu nyingine.