Mourinho alimponda Mreno mwenzake huyo kwamba si ‘Ronaldo halisi’ akimfananisha na fowadi wa zamani wa Brazil, Ronaldo de Lima.
Mourinho alitoa kauli hiyo siku chache kabla ya
mechi baina ya Chelsea na Real Madrid iliyofanyika nchini Marekani, kitu
ambacho Ronaldo alikuja kukijibu ndani ya uwanja kwa kufunga mabao
mawili katika ushindi wa 3-1 na hivyo kumfunga mdomo bosi wake huyo wa
zamani.
Katika kutimiza lengo lake la kumzima Mourinho,
Ronaldo alikumbana na vikwazo vingi uwanjani, ikiwamo kuvumilia maumivu
baada ya kuonekana kifundo cha mguu wa kushoto kuvuja damu mchezoni.
Hadi filimbi ya mwisho katika mchezo huo, Ronaldo alimzima bosi wake huyo wa zamani.