Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani mama Lily Munanka (kati) akiwakaribisha Masanja na Shilole wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa…
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani mama Lily Munanka (kati) akiwakaribisha Masanja na Shilole wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa kiswahili Marekani, Bwn. Baraka Daudi (kushoto) na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ya maandalizi Bwn. Idd Sandaly Ubalozini hapo Jumanne July 2, 2013 walipokwenda kumtembelea na kufanya kikao kwa kumuelezea Kaimu Balozi maandalizi ya sherehe hii itakayofanyika Jumamosi July 6, 2013 yalikofikia.
Kutoka kushoto ni Baraka Daudi, Kaimu Balozi mama Lily Munanka, Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly, Shilole na Masanja Mkandamizaji wakiongea jambo walipokua Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC.
Masanja na Shilole katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
Shilole na Masanja walipotembelea ofisi za Community Mult Services, Inc zilizopo Silver Spring, Maryland.
Kutoka kushoto ni Mr. Watson, Ms Patricia, Jamila, Shira, Mrs Reese, Shilole, Masanja na Baraka katika picha ya pamoja.
Mussa Shedafa katika picha ya pamoja na wasanii