JANA
Nay wa Mitego alikuwa akiandika ujumbe wenye mafumbo kwenye Instagram
na baada ya kuusoma ndani ya mistari ilibainika kuwa huenda mambo si
mazuri kati yake na mpenzi wake ambaye hivi karibuni alikuwa akitarajia
kumzalia mtoto lakini mimba ikaharibika.
Nay ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Munisi, jana alianza kwa
kuandika ujumbe huu: Sasa mapenzi basi# by diamond Platnumz..!! Single
boy# Ally Kiba#966’
Baada ya muda kidogo aliandika tena:
"Niko ivi,,, nikikupenda nakupenda kwa asilimia 100# na kila m2 atajua
juu ya upendo wangu kwako..!! Bt ukizingua nakuacha na ninakusahau kwa
asilimia 200# na kwa muda mchache 2.
"Nikiamua huwa sirudi nyuma..!!# Mwanamke mjinga ataivunja ndoa yake kwa mikono yake ye mwenyewe# by Linex.#966’