Tuesday, August 27, 2013

HABARI MPYA KUTOKA KWA MBUNGE H.KIGWANGALLA USIKU HUU KUHUSU MADAWA YA KULEVYA


 
SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA: Nawashukuru Raia wema waliojitoa kuniletea taarifa za mitandao na watu wanaohusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Ninaendelea kuzifanyia utafiti taarifa hizi ili kubaini ukweli bila mashaka makubwa kabla sijaamua kuziweka wazi bungeni, Dodoma kama nilivyodhamiria. Kwa hakika sintotaja majina ya watu kwa kuwasingizia, nitahakikisha nina ushahidi ama maelezo ya kina kuhusiana na kila nitakayemtaja na namna ya ushiriki wake. Ninalenga pia kukusanya taarifa itakayozikua na kubainisha kwa uwazi mtandao ulivyo na namna wanavyofanya biashara hii kuanzia wanavyoingiza, wanavyoficha, aina za madawa na mahala wanapopeleka, pia jinsi wanavyosambaza nchini na nchi nyingine. Nazidi kuwasihi wengine wote wenye taarifa zozote zile zinazoweza kusaidia harakati za kupambana na biashara hii haramu wasisite kuzifikisha kwangu.