FILAMU ya kimataifa iliyoandaliwa Swahilihood na kwa ushirikiano wa nchi 6 inayojulikana kwa jina la Going Bongo imekamilika mwezi wa nane, kwa sasa watayarishaji wapo katika mikakati ya kufanya uzinduzi ambao utatangazwa wakati wowote, akionge na FC mmoja wa watengenezaji wa filamu hiyo Nick Marwa amesema kuwa filamu hiyo ni kazi ambayo inaweza kuwa ni ya kwanza kwa kushirikisha watalaam kutoka nchi mbalimbali.
Nchi zilizoshirikiana katika utayarishaji wa filamu hiyo ni Tanzania, Italy, Kenya, Marekani, UK, Turkey na filamu ya Going Bongo ilianza kurekodiwa Marekani katika jiji la Los Angeles, California na kuja kumaliziwa Tanzania wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ni Ernest “Napoleon” Rwandalla kinara wa filamu, Ashley Olds huyu kutoka Marekani.
.
Watayarishaji wa filamu ya Going Bongo ni Nick Marwa, Ernest Napoleon, Bryan Ronalds, mswada umeandikwa na Ernest Napoleon Rwandallah na Gregory Zyment wapiga picha ni mwanadada Leslie Bumgarner kutoka Marekani akisaidiwa na George Mboya kutoka Kenya, Filamu imeongozwa na Dean Ronalds.
Kulingana na makampuni ya usambazaji kununua filamu kwa kiwango cha chini inawezekana ikawa ni vigumu kuweza kununua filamu hiyo ambayo bajeti yake ya utayarishaji pekee ni milioni 450 za Kitanzania, filamu hiyo inatarajiwa kuonyeshwa Toronto Canada na baadae katika nchi zote washirika katika kutengeneza. Pia unaweza kuangalia Trailer kwa kupitia www.vimeo.com/71947975