Wednesday, August 7, 2013

Cocacola wamkodishia Diamond ‘private jet’ peke yake kutoka Nairobi hadi Dar


Kufuatiaa tukio la moto lililo tokea leo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA jijini Nairobi, Kenya na kusababisha uwanja huo kufungwa kwa muda na kumfanya Diamond Platnumz aliyetua alfajiri ya leo akitokea Afrika Kusini kukwamwa, Cocacola wamemchukulia ndege binafsi itakayomleta Dar es Salaam.
Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha wakati akipenda kwenye ndege hiyo ambamo atakuwa peke yake na rubani.

“Had no choice than dat, coz i miss my mum and Baby lyk crazy… @ Wilson Airport Nairobi… can’t wait to see you @rommyjones #I #MySelf #AloneInTheJet #CocaBoy …. #Cocacola Mmetisha sana, asanteni sana,” ameandika.

Diamond ni balozi wa Cocacola.

Hizi ni bei za kukodi ndege binafsi nchini Kenya.

Air Charter Rates at HKNW

Turbo-Props: $1,200 – $1,800/hr

Light Jets: $1,900 – $2,650/hr

Mid-size Jets: $2,700 – $3,400/hr

Large Jets: $3,600 – $7,800/hr