Friday, July 5, 2013

RAIS KIKWETE KUWA REFA MECHI YA WABUNGE‏ WA SIMBA NA YANGA


Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalo fanyika Jumapili hii, Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aidha, Rais atahutubia katika tamasha na pia atakuwa refa wa mechi za wabunge wa Yanga na Simba.