Saturday, July 27, 2013

RAIS KIKWETE AMTEMBELEA HOSPITALI MMILIKI WA HOME SHOPING CENTER ALIYEMWAGIWA TINDIKALI.

Mmiliki wa Homeshoping centre na Msasani City mall kalazwa South Afrika July 26 2013 JK Kamtembelea
Said anatajwa kuwa mmiliki wa maduka ya Home shopping centre na pia mmiliki wa jengo jipya ambalo limechukua headlines Dar es salaam la Msasani City Mall ambalo ndani yake kuna maduka ya nguo na viatu.. yote yakiwa yanamilikiwa na yeye tu.

Siku kadhaa zilizopita alimwagiwa tindikali na mtu ambae hakufahamika ambapo muda mfupi baadae alikimbizwa hospitali Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ambapo Rais Jakaya Kikwete mtu wa watu ni miongoni mwa waliokwenda kumjulia hali kama unavyomuona kwenye picha.
Moja kati ya Magazeti pendwa wiki hii yalitoa ripoti kwamba Said ndio anatajwa kuwa tajiri kuliko wafanyabiashara wote Kariakoo Dar es salaam.