Saturday, July 27, 2013

MIENO KUZIBA PENGO LA VICTOR WANYAMA, CELTIC


Sasa ikiwa ni wiki kadhaa tangu kiungo huyo wa Kenya kuondoka, kocha wa Celtic Neil Lennon, amesema Wanyama alikuwa ndio kiungo wake bora wa ushambuliaji kwenye timu yake na sasa wanahitaji mbadala wake. 
Kutokana na hilo sasa zimeibuka taarifa kwamba kocha huyo ambaye ni nahodha wa zamani wa Celtic anamuwania kiungo mwingine kutoka Kenya Humphrey Mieno. Mieno ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Azam FC  inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Tanzania. 

Celtic, itabidi ifanye haraka kumsaini mchezaji huyo wa Azam FC kwa kuwa kuna vilabu vingi barani Afrika kama miamba ya soka ya Tunisia Esperance na Club Africain zinamuwania kwa nguvu mchezaji huyo ambaye alihamia Azam akitokea Sofapaka ya Kenya.

Mpaka sasa sio Celtic wala Azam FC ambazo zimethibitisha kuhusu taarifa hizi.