POLISI katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wamemkamata mwanamke mmoja aitwaye Rozi Amel (45) ambaye ni mfanyabiashara akiwa na milipuko, baruti na viunganishi vyake pamoja na silaha mbili za moto huko Salasala IPTL jijini Dar. Haikuweza kufahamika mara moja milipuko hiyo alikuwa akiipeleka wapi. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura upelelezi bado unaendelea.
Friday, July 26, 2013
POLISI YAKAMATA MILIPUKO NA SILAHA JIJINI DAR
at
10:28 AM