Friday, July 5, 2013

MAN CITY YAMFUNGIA KAZI PEPE WA REAL MADRID

CLUB ya Man City imeongeza kasi katika nia yake ya kumnasa beki Mreno anayekipiga Real Madrid, Pepe, 30.

CLUB ya Man City imeongeza kasi katika nia yake ya 

Bosi mpya Etihad, Manuel Pellegrini amemfanya beki huyo anayependwa Bernabeu kuwa lengo lake kuu kwenye ngome kiangazi hiki.

Pellegrini anataka beki mpya wa kati baada ya Kolo Toure kuhamia Liverpool na Joleon Lescott akibakisha mwaka mmoja tu katika mkataba wake.

Lakini miamba hiyo ya Hispania inaonekana kutaka karibu pauni milioni 20 kuweza kumwachia Pepe.

Pellegrini anamuweka Pepe katika daraja la juu, kama mmoja wa mabeki bora katika La Liga, licha ya sifa yake ya kuwa mwepesi wa kupandwa hasira.

Wakati huo huo, Rais wa Sevilla, Jose Maria del Nido amethibitisha kuwa tayari kumpiga bei mshambuliaji wake Mhispania Alvaro Negrado, 27, mwenye thamani ya pauni milioni 21 baada ya City kuonyesha nia ya kumtaka.

Alisema: “Kuna klabu mbili England ambazo zinamtaka na kuondoka kwake kunaweza kutokea.”