Wednesday, June 26, 2013

NIMEWAGUNDUA WABAYA WANGU NDANI YA CHADEMA"...LWAKATARE

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, WILFRED LWAKATARE amesema kuwa siasa za chuki na majungu ndani ya chama hicho zimetawala hali inayokwamisha harakati mbalimbali za kisiasa za chama hicho hadi kufikia kusalitiana hatua iliyofanya hata mipango mbalimbali kukwama. Alitolea mfano wa video aliyorekodiwa kuwa ililenga kumuumbua yeye
Aidha taarifa za ndani za chama kutolewa nje kwa maadui wa CHADEMA kisiasa nyingi zinatolewa na viongozi na wanachama wasio waaminifu.

Hayo aliyasema wakati wa Mkutano na wanachama wa chama hicho uliofanyika Juni 19, 2013 kwenye Viwanja vya mashujaa maarufu kwa jina la Mayunga mjini Bukoba.

Aidha, Lwakatare aliwaambia wananchi waliokusanyika katika viwanja hivyo vya mashujaa kuwa nafasi yake na Ukurugenzi wa Ulinzi na Usalama inamsaidia kuwagundua maadui wake