Monday, July 1, 2013
FAHAMU USIYOYAJUA KUHUSU MALCOM X...
at
4:24 AM
PATA HISTORIA FUPI YA MALCOM X
Malcom x (amezaliwa may 19, 1925-na kufa februari 21,1965) pia anajuliakana kwa jina la EL-hajj malik el-shabbaz.malcom x alikuwa ni mwa amerika mweusi waziri wa kiislamu(African American muslim minister),mhadhiri(public speaker) na mpiganaji wa haki za kibinadamu.kutokana na dhamira yake kuu malcom x alikuwa ni muelewa na mpiganaji hasa katika haki za wa amerika weusi(rights for African americans) kwa kuwapa wakati mgumu wazungu dhidi ya haki ya wa amerika weusi. wahasimu wa al-hajj malik el-shabbaz walimzushia na kumtuhumu kuwa na sera za ubaguzi wa rangi (racism) na kukiuka sharia.mpaka leo katika dunia ya sasa malcom x anazungumziwa kama miongoni mwa wakubwa na wenye ushawishi mkubwa hasa zaidi katika historia ya wa amerika weusi.
Malcom x alizaliwa Omaha,Nebraska.malcom x alipofikisha umri wa miaka 13, baba ake mzazi alifariki dunia huku mama ake mzazi akiwa anaugua uchizi na ikabidi apelekwe katika hospitali ya vichaa.katika utoto wake malcom x, hasa zaidi kwa mafundisho aliyopata kwa baba yake kuhusu wasifu wa watu weusi(black pride) ujamaa wa kujitegemea na uzoefu aliokuwa nae kuhusu ubaguzi wa rangi, umechangia nafasi kubwa mno hasa zaidi katika maisha yake ya ukubwani ya malcom x. kwa kipindi chote malcom x alikuwa akilelewa katika vituo vinavyotoa msaada wa malezi (foster homies),malcom x akahusishwa na uhalifu huko Boston and new York. Katika mwaka wa 1945, malcom x alihikumiwa miaka nane mpaka kumi kwenda gerezani.
Wakati yupo gerezani malcom x akawa miongoni mwa wanachama wa NATION ISLAM. Wakati wa muda wake wa kutoka gerezani ulipofika 1952, akawa miongoni mwa kiongozi wa kitaifa na mzungumzaji mkuu wa chama hicho.ndani ya miaka kadhaa iliyofuata malcom x akawa kama kioo cha jamii nzima ya NATION ISLAM . kutokana na baadhi ya mtafaruku kati ya malcom x na ellijah muhamad ambaye ndio alikuwa kiongozi mkuu wa Nation islam,ikampelekea malcom x kutoka katika kikundi hicho machi 1964.
Baada ya kuondoka katika kikundi hicho cha Nation islam, malcom x akawa miongoni mwa wa sunni (sunni muslim) na ikampelekea kwenda kuhiji mecca. Katika misafara yake yote alitembea zaidi Africa na mashariki ya kati (middle east), na kufanikiwa kuanzisha misikiti ya kiislam, vikundi vya kidini (religious organization) na black nationalist organization of Afro-American unity. Haikumaliza hata mwaka mmoja toka aondoke katika kikundi cha nation islam, malcom x aliuliwa (assassinated) wakati akitoa hutuba ndani ya jiji la new York.
KUKUTANA NA CASTRO NA VIONGOZI WENGINE WA ULIMWENGUNI
Ndani ya septemba 1960, fidel castro alikuja new York hasa zaidi kuhudhuria kikao cha umoja wa umoja wa mataifa (United Nations General Assembly). Castro pamoja na kundi lake walifikia katika Hotel Theresa ndani ya Harlem. Malcom x alikuwa anajulikana kama ni miongoni mwa wanachama wa kamati ya Harlem amabaye aliteuliwa katika kuwakaribisha wakina castro. Castro alivutiwa sana na malcom x na akaomba kikao cha faragha na malcom x (private meeting).katika kipindi cha kikao hicho cha umoja wa mataifa(General Assembly meeting),malcom x pia aliweza kukaribishwa na viongozi tofauti wa ubalozi katika nchi za kiiafrica, ambapo aliweza kukutana na wakuu wa nchi tofauti pamoja na viongozi wengine pia.., kama vile Gamal Abdel Nasser wa Egypt, Ahmed sekou Toure wa Guinea, na Kenneth Kaunda wa Zambian African National congress
-