Friday, July 19, 2013

BREAKING NEWS: KOCHA WA FC BARCELONA KUJIUZULU SAA CHACHE ZIJAZO

Kocha wa Barcelona Ttito Vilanova .
Taarifa toka nchini Hispania zinasema kuwa klabu bingwa ya Hispania Fc Barcelona inatarajia kutangaza kuachia ngazi kwa kocha wake Tito Villanova ndani ya saa chache zijazo .Taarifa toka vyanzo vya kuaminika ikiwemo kituo cha michezo cha Uingereza Skysports , Tito Vilanova amefikia uamuzi huo baada ya kufanyiwa vipimo vya afya ambapo imegundulika kuwa tatizo lake la saratani ya tezi zilizoko kooni mwake limejirudia tena na anatarajiwa kwenda nchini marekani kupewa matibabu ya kitaalamu zaidi .
Ttito Vilanova aligundulika kuwa na tatizo hilo miaka mitatu iliyopita ambapo alifanyiwa upasuaji na ilidhaniwa kuwa amepona kabisa kabla ya tatizo hilo kujitokeza tena kuelekea mwishoni mwa mwaka jana ambapo alilazimika kuiacha timu mikononi mwa kocha msaidizi Jordi Roura ambaye alichukua nafasi yake. Villanova alirejea mwezi januari na safari hii atalazimika kuachia ngazi kwa muda mrefu ili atibiwe