Thursday, July 4, 2013

BOMOA BOMOA YA POMBE MAGUFULI YAANZA.....JENGO LA BUSINESS PARK ( GREEN ACRES ) LABOMOLEWA

 Baada Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa wenye majengo yaliyo pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kubomoa wenyewe majengo yao ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kuonekana yakisua sua, hatimaye leo ameanza rasmi kazi ya kubomoa kwa Greda katika majengo ya wale walioonekana kukaidi agizo hilo. 


Katika kutekeleza agizo hilo zoezi hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo eneo la Victoria ambapo hadi hivi sasa zoezi hilo bado linaendelea pande hizo chini ya usimamizi ya Askari