Tuesday, July 30, 2013

BODI YAKANUSHA UVUMI KUWA WALIOOMBA MKOPO WA ELIMU WANAPASWA KUJIANDIKISHA UPYA...!

Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.

Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.

Aidha Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni
mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz

Tangazo hili limetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU